Saturday, March 22, 2014
0
Bunge la Kenya lenye wabunge wengi wanaume limeidhinisha mageuzi yenye utata katika mswada wa ndoa ambayo yatawapa wanaume usemi zaidi katika familia na uhusiano mwingine katika jamii.
Wabunge wanaume waliungana kupitisha mageuzi hayo ambayo yataathiri....
pakubwa familia kwa ujumla
Wabunge wanaume walipitisha mswada mpya wa ndoa baada ya kuufanyia mageuzi na kuruhusu wanaume kuoa zaidi ya mwanamke mmoja bila ya kushauriana na mke wa kwanza. .
Wabunge wanawake waliondoka katika kikao hicho kwa hasira wakiahidi kuubadili mswada huo.
Pia sehemu za sheria ya ndoa ambazo zinasema kuwa wanandoa waweze kugawana mali yao wanapoachana imelegezwa.
Wanawake wameahidi kubadili kufutilia mbali mswada huo

Mswada wenyewe awali uliruhusu wanaume kuoa wanawake zaidi ya mmoja lakini ukasisitiza kuwa mke wa kwanza sharti ashaurie kabla ya mumewe kuoa mke wa pili au wa tatu.
Mmoja wa wabunge wanawake alisema kuwa ni muhimu mageuzi hayo katika mswada huo kutupiliwa mbali kwa ajili ya kulinda familia.
''Ni muhimu kumuomba mkeo wa kwanza ruhusa kabla ya kuoa mke wa pili,'' alisema mbunge huyo. Lakini mbunge mmoja mwanamume, Benjamin Washiali, alisisitiza kuwa yeye ni mtoto wa mke wa pili katika familia yao. ''Ikiwa sheria hii ingekuwepo mimi nisingezaliwa.''
Wabunge wengi wanaume wamesema kuwa ni jambo la kawaida kwa wanaume wa kiafrika kuwa na wake zaidi ya mmoja.
Wanawake bungeni sasa wanasema watajitahidi kuhakikisha kuwa mswada huo unatupiliwa mbali.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA