Wednesday, March 12, 2014
0
Mwanamume mmoja aliyeishi jela kwa zaidi ya miaka 25 akisubiri hukumu ya kifo nchini Marekani, ameachiliwa huru baada ya mahakama kubatilisha uamuzi wa mahakama kuwa alikuwa na hatia ya mauaji yaliyotokea mwaka 1983.
Glenn Ford, 64, alikuwa jela akisubiri hukumu ya kunyongwa tangu..
mwaka 1988 mwezi Agosti.
Mahakama wakati huo ilimpata na hatia ya mauaji ya Isadore Rozeman aliyekuwa na umri wa miaka 56 akiuza mikufu. Bwana Ford alikuwa mfanyakazi wake wakati huo.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa ni mmoja wa wafungwa waliohukumiwa kifo kwa muda mrefu nchini humo na kuachiliwa.
Glenn alisema kuwa anahisi vizuri sana kwamba ameachiliwa.

Makosa kwenye kesi

  • Hakuna silaha yoyote ilipatikana na hapakuwa na mashahidi katika kesi hiyo.
  • Mwanamke aliyemhusisha Ford na mauaji hayo alisema kuwa ushahidi wake haukuwa wa kweli na kwamba alidanganya.
  • Mawakili wa Ford walioteuliwa na mahakama hawakuwahi kuendesha kesi ya mauaji
  • Bwana Mmarekani mweusi alihukumiwa na jopo la wazungu waliopendekeza auawe.
Alisema ana maudhi ndani ya moyo wake kutokana na kufungwa bila hatia kwa kitu ambacho hakukifanya na kuwa amepoteza muda wake mwingi jela.
"miaka 30 ya maisha yangu. Siwezi kufanya mambo ambayo ningefanya nikiwa na umri wa miaka 35, 38 au 40. Mwanangu nilipofungwa jela alikuwa mtoto sasa ni mtu mzima na watoto wake.''
Jaji aliymwachilia huru bwana Ford, Ramona Emanuel alisema Jumatatu kuwa kulikuwa na ushahidi mpya kuonyesha kwamba Bwana Ford, hakuhusika na mauaji hayo.
Makosa mengi yalipatikana katika kesi dhidi ya Ford kama yalivyoelezwa na vyombo vya habari nchini Marekani.
Inaarifiwa kuwa kesi ya Ford iliendeshwa na mawakili ambao hawakua na ujuzi wa kazi.
SOURCE BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA