Wednesday, March 19, 2014
0

Mkuu wa idara ya kupokea malalamishi ya umma, Bi Thuli Madonsela, hivi leo anatarajiwa kutoa ripoti ya idara hiyo kuhusu uchunguzi wa iwapo Rais Jacob Zuma alihusika katika ufisadi ambapo inadaiwa kuwa alitumia pesa za umma dola milioni
ishirini kukarabati boma lake la kifahari liililopo katika kijiji cha...
Nkandla alikozaliwa.
Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vimedokeza kuwa Rais Jacob Zuma amefanya mashauriano na Bi Madonzela, hivi
karibuni wakati ambapo chama tawala cha ANC kimetoa wito kwa wanachama wake kupuuza repoti hiyo ya Bi Madonzela iwapo itamshirikisha Rais Zuma.
Boma la Nkandla la kibinafsi la Rais Zuma lina nyumba kadhaa, na limewekwa mitambo ya kisasa ya kiusalama ili kumlinda
Rais.
Kulingana na mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa, Waziri wa Ujenzi wa Kazi za Umma nchini humo Nthula
Tsinthesi, ilikuwa muhimu kukarabati boma hilo kwa kiasi hicho cha pesa kwa sababu boma hilo limewahi kuvamiwa mara
tatu ya wahalifu wasiojulikana.
Ukarabati huo wa boma la Rais ambao sasa umenukia kuwa kashfa umewafanya wengi kuhoji iwapo bwawa la kuogelea
la kisasa lililojengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa ni sehemu ya usalama unaotajwa.
Na pia kumekuwepo na habari zinazodaiwa kuwa katika ripoti hiyo ambazo zinadai kuwa Rais Zuma mwenyewe alitoa
amri pesa za umma kutumiwa, ambacho ni kinyume cha kanuni za kazi yake.
Raisi Zuma akicheza Ngoma za kiutamaduni kijijini kwake..
Raisi Serebuka Serebuka..

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA