Wanawake wawili, Jumatatu walizuiliwa kwa saa 3 na
mahakama moja nchini Uganda kwa kuingia mahakamani wakiwa wamevalia
'Mini Skirt'.
Hii ni baada ya jaji aliyekuwa mahakamani humo kusema kuwa wanawake hao...
walikuwa wamevalia nguo zisizofaa.
Kwa mujibu wa taarifa kwenye mtandao
wa Daily Nation, nchini Kenya, Bi Prosy Nasuna aliyekuwa amemshitaki Bi
Jane Nabukenya kwa kukosa kumlipa deni lake la shilingi milioni 3 za
Uganda wote walisemekana kutovalia nguo za heshima na kutatiza kikao cha
mahakama.
Walipoingia mahakamani katika eneo la Bukomansimbi wiki jana Prosy pamoja na mshitakiwa walijikuta matatani.
Kabla ya kuchukuliwa hatua kwa mavazi yao, watu
walipiga mayowe mahakamani humo wakisema kuwa wawili hao walikuwa
wamevalia visivyo kulingana na sheria iliyopitishwa mwezi jana kuhusiana
na kupiga marufuku mavazi fupi.
Sheria hiyo inasema kuwa yeyote atakeyeonyesha
sehemu za siri za mwili wake hadharani na kusababisha hisia fulani
miongoni mwa watu, anakuwa amekiuka sheria.
Minong'ono na kelele za watu zilisababisha
hakimu kuamuru kukamatwa kwao kwa kwenda kinyume na sheria na pia kwa
kuhujumu mahakama.
Alisema kuwa kesi ilikosa kuendelea kutokana na
mavazi yao na kwa hivyo kosa lao lilikuwa kusababisha usumbufu
mahakamani kwa kuvalia 'Mini Skirt'
Hakimu aliwahukumu jela masaa 3 wanawake hao na kuahirisha kesi yao hadi tarehe 13 mwezi Machi.
SOURCE BBC SWAHILI |
0 comments:
Post a Comment