Sunday, April 20, 2014
0
Maafisa wawili wa polisi nchini Misri wameuawa kufuatia shambulizi la risasi katika barabara kati ya mji wa Cairo na mfereji wa Suez.
Shambulizi hilo linajiri siku mbili baada ya afisa mwengine wa polisi kuuawa katika mlipuko wa bomu katikati ya mji mkuu wa Cairo.
Wanamgambo wa kiislamu wametishia kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama vya taifa hilo.
Mamia ya wanajeshi pamoja na polisi wameuawa tangia jeshi limuondoe madarakani aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Mohammed Morsi mnamo mwezi Julai.
Zaidi ya wafuasi elfu 15 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood wamefungwa jela.
Mamia ya wengine wamepewa hukumu ya kifo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA