Thursday, April 10, 2014
0
 Amini usiamin. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine. Linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, mkoani Iringa Bw.Kenny Mwangoka.
Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika vibaya. Jitihada zake za kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.
"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema, na kuongeza kuwa baada ya.... matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.
"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema, na kuongeza kuwa  atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane mwaka huu kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti.
 Na Francis Godwin, Iringa

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA