Tuesday, April 22, 2014
0
Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke la kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.
Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya teke hilo, wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelidaka kombora lililopigwa langoni mwake, lakini mshambuliaji alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.
Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa Bongoville ambalo ni umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA