Wednesday, April 30, 2014
0
Serikali ya Kenya imelalamikia serikali ya Italia kuhusu tukio la mwanariadha mkenya kuanguka katika mkondo wa mbio za Marathon.
Kupitia kwa waziri wa michezo Hassan Wario, Kenya inataka kujua kwa nini maafisa wa mbio hizo walichelewa kumsaidia Eliud Magut na kumuacha kuendelea kukimbia ilihali ilikuwa wazi alikuwa anatatizika
Mwanariadha huyo alianguka mara tatu akiwa amesalia na mita miatatu sabini kumaliza mbio hizo zilizofanyika katika eneo la Padua.
Mashabiki pamoja na maafisa wa mbio hizo walikuwa wanamshangilia na kumsihi Eliud Magut kuendelea kukimbia licha ya kuanguka mara tatu akijikaza kumaliza mbio hizo.
Wasiwasi umeibuka kuhusu kwa nini waandalizi wa mbio hizo walimruhusu Magut kuendelea kukimbia licha ya kuanguka chini mara tatu kando ya mkondo wa mbio na kabla ya kuleta ambiulensi kumkimbiza hospitalini.
Magut aliwahi kushinda mbio za nyika za Cannes Marathon nchini Ufaransa mwaka 2012 na kumaliza wa pili katika mbio za amani mjini Kigali Rwanda.
Magut alikuwa anakimbia akitarajia kumaliza wa tatu nyuma ya Fatna Maraoui na mwenzake Pharis Kimani aliyemaliza katika nafasi ya pili.
Ripoti zinahoji sana kwa nini maafisa wa mbio hizo hawakuchukua hatua zozote licha ya mafadhaiko aliyokuwa anapata Magut.
Maafisa wa shirikisho la riadha nchini Kenya wamesema kuwa wanachunguza kisa hicho , wakisema kuwa ni jambo la kusikitisha.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA