Tuesday, September 04, 2012
0
Rimsha Masih
Kesi ambayo msichana mmoja wa kikristo alikamatwa nchini Pakistan chini ya sheria tatanishi ya kukufuru dini, imeakhirishwa huku msichana huyo akiendelea kuzuiliwa.



 

 
Taarifa zinasema kuwa mgomo wa mawakili ulitatiza kesi hiyo kuweza kuendelea hii leo.
Rimsha Masih alishtakiwa kwa madai ya kuchoma kurasa za Quran.
Lakini mhubiri mmoja wa kiisilamu , Khalid Chishti, amekamatwa kwa njama ya kujaribu kumlimbikizia msichana huyo makosa ambayo hakuyafanya.
Mashahidi katika kesi hiyo akiwemo msaidizi wa mhubiri huyo, aliambia wendesha mashtaka kuwa walimuona mhubiri huyo akiongeza kurasa za Quran kwenye mfuko aliokuwa anaubeba msichana huyo ukiwa na karatasi zilizochomwa.
Hatua ya msichana huyo kuzuiliwa imezua hisia kali kutoka kwa makundi ya kikristo pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu na vile vile kuna taarifa zenye utata kuhusu umri wake na hali yake ya kiakili.


Rimsha, katika picha ya kuchora!


Wakristo wakiandamana ili mtoto Rimsha (11) aachiliwe..


Mtoto Rimsha akiwa na mmoja wa mawakili waliojitolea kumsaidia!

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA