Wednesday, September 19, 2012
0



Maafisa wa utawala mjini Cairo, wameamuru kukamatwa kwa wakiristu saba wa kikopti raia wa Misri wanaoishi nchini Marekani kwa kuhusika na utengezaji wa filamu iliyozua ghadhabu miongoni mwa.........

 waisilamu wengi kote duniani.
Filamu hiyo ambayo inamkejeli mtume Muhammad ilizua ghasia na kero katika mataifa ya kiislamu kwa namna ilivyomdhihaki Mtume.
Hata hivyo haijabainika mtunzi wa filamu hiyo lakini imehusishwa na wakristo wa kikopti wanaoishi nchini Marekani.Kibali cha kumkamata mchungaji Terry Jones nchini Marekani pia kimetolewa.
Mwanamke mmoja na wanaume saba akiwemo Jones, wanatuhumiwa kwa kuitusi dini ya kiisilamu na kuchochea ghasia za kidini , kwa mujibu wa taarifa za mwendesha mkuu wa mashtaka.
Taarifa hiyo ilisema kuwa shirika la polisi wa kimataifa la Interpol, watafahamishwa kuhusu vibali hivyo.Ombi pia litatolewa kwa maafisa wa kisheria nchini Marekani. Inaarifiwa kuwa ikiwa wote waliotuhumiwa watapatikana na hatia huenda wakahukumiwa kifo.

Mchungaji Terry Jones, naye pia kukamatwa..

Terry Jones

Terry Jones

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA