Monday, September 17, 2012
0



Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema kuwa serikali yake itampiga marufuku mhubiri mmoja tatanishi kuingia nchini humo....

Kasisi Terry Jones, anayesifika kwa vitisho vyake vya kuiteketeza Quran nchini Marekani, amealikwa kuhutubia mikutano kadhaa za mashirika ya watu wenye siasa kali.
Bi Merkel alisema kuwa ikiwa mpango wake utafanikiwa hatapewa visa kuingia nchini humo.
Bwana Jones amesema kuwa anaunga mkono filamu iliyozua kero miongoni mwa waisilamu kote duniani hasa Mashariki ya Kati.
Mwandishi wa BBC mjini Berlin, anasema kuwa makundi yenye siasa kali nchini Ujerumani ambayo yamemwalika, yanataka kuionyesha filamu hiyo hadharani.
Kasisi Terry Jones

Kasisi Terry Jones

Kasisi Terry Jones

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA