Tuesday, September 11, 2012
0


Ilikuwa tareha 11 septemba ya mwaka 2001, ambapo watu  19 wanaohusika na kundi la Al-Qaeda waliteka ndege nne za abiria, na kuzitumia kama vyombo vya milipuko (mabomu) ili kupiga  sehemu walizozilenga huko Marekani.
 


Ndege mbili zilipiga ghorofa pacha za World Trade Centre huko New York City, ndege nyingine ilipiga ofisi za Pentagon pembeni  kidogo mwa Washighton D.C. Ndege ya nne na ya mwisho ilianguka huko Pennsylvania.
Tukio hilo lilisababisha uharibifu mkubwa wa mali na upotevu wa maisha wa watu zaidi ya 3,000 ambapo kati yao 400 walikuwa askari na waokozi wa kikosi cha uokoaji.. Ni miaka zaidi ya 11 sasa lakini machungu kwa wale waliopeteza wapendwa wao bado yangalipo.
MUNGU UTUSAIDIE, naomba uifanye Dunia iwe sehemu salama ya kuishi, tafadhali nawe unaesoma habari hii kumbuka KUOMBA na MUNGU  AKUBARIKI..




 


0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA