Monday, January 07, 2013
0


KANISA la Moravian Duniani lenye Makao Mkuu yake nchini Norway, limeingilia kati mgogoro wa kanisa lake Jimbo la Mashariki na Pwani Tanzania kwa kutaka kuondoa......


 kesi inayowafanya walumbane mahakamani.
Mgogoro huo ulizuka baada ya kuondolewa nyadhifa na kusimamishwa kazi, Mwenyekiti wa Halmashauri Jimbo hilo, Clementi Fumbo na wenzake saba.
Fumbo na wenzake saba walifungua kesi ya madai namba 222 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam wakipinga kuondolewa madaraka na kusimamishwa kazi.
Katika kesi hiyo, iliyopangwa kusikilizwa na Jaji Augustine Mwarija, Desemba 6, mwaka huu, Fumbo na wenzake saba wanaiomba Mahakama iamuru walipwe Sh500 milioni kama fidia na gharama za kesi.
Kanisa la Moravian duniani ambalo makao makuu yake yapo nchini Norway limeshtushwa na mgogoro huo ambao ulipelekwa mahakamani.
Kanisa hilo limetuma ujumbe unaoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kanisa hilo la Moravian dunia, Mchungaji Nosigwe Buya na Mtendaji wake Mkuu wa Kanisa hilo, Mchungaji Jogan Boytrel.
Ilidaiwa kuwa wajumbe hao, walipofika hapa nchini walifanya vikao tofauti tofauti na kufikia uamuzi kuwa ifikapo Januari 15, 2013 pande zote mbili zenye mgogoro ziwe zimekwishaelewana na kuwapelekea ripoti.
Iliendelea kudaiwa kuwa iwapo watashindwa kufika muafaka na kuelewana Februari Mosi,2013, ujumbe huo utarudi kutoa uamuzi na kwamba wakielewana watapewa jimbo kamili.
Katika kesi hiyo, Mchungaji Fumbo kupitia wakili wao, Benjamini Mwakagamba wa Ofisi ya Mawakili ya BM, wanaiomba mahakama hiyo, itamke kuwa uamuzi ambao uliowaondolea madaraka na kuwasimamisha kazi ya kikao cha Sinodi cha Oktoba 5, mwaka 2012, kilichokaa mkoani Morogoro ni batili kwa kuwa uamuzi huo ulitolewa bila ya wadaiwa kupewa haki ya msingi ya kusikilizwa.
Fumbo na wenzake Mchungaji Fred Lwitiko, Mchungaji Mosted Kibona, Mchungaji Nyambilila Lwaga, Nelson Ngajiro, Devis Mwaikambo, Mathew Mwasiposya na Aliko Mwakatumbula kwa pamoja wanadai kuwa wadaiwa ambao ni Mchungaji Saul Kajula, Mchungaji Clement Mwaitebele, Halmashauri Kuu ya Jimbo la Moravian Mashariki na Bodi ya wadhamini ya kanisa la Moravian Jimbo la Rungwe kwa pamoja na kwa nyakati tofauti walitoa uamuzi wa kumsimamisha na kumfukuza kazi ya uenyekiti wa halmashauri ya Jimbo la Mashariki Mchungaji Fumbo na kumuondoa kwenye nafasi ya mweka hazina Mchungaji Lwaga.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA