Monday, January 14, 2013
0



UTANGULIZI:                                                   
 Yeremia 25:34-37 “Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za.....
 
kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.  Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.  Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kupiga yowe kwao walio hodari katika katika kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao.  Na mazizi yenye amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA”.
Katika mkesha wa maombi ya KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA (KLPT) Parish ya Mbezi Luis, Jimbo la Kinondoni Dar Es Salaam, uliofanyika usiku wa tarehe 12 kuamkia tarehe 13 mwezi Oktoba, 2012 hapa Parishini, Neno la BWANA lilishuka na kunilenga mimi MCHUNGAJI BENT M. DONGWE likisema:
“Nakutuma wewe Mchungaji BENT M. DONGWE, nenda kaseme na Wachungaji na Wahubiri wa Kanisa la Tanzania kupitia vyombo vya habari, Television, Redio na Magazeti uwaambie Bwana wa Majeshi asema hivi; Acheni mara moja kuhubiri watu fedha Makanisani, wahubirieni watu Neno langu, acheni kuwakata Kondoo wangu mikia, acheni kuwakusanya Kondoo wangu ili kushibishana matumbo yenu Asema Bwana wa Majeshi”.
Ezekieli 34:1-10 “Neno la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasiwachungaji kuwalisha kondoo? Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo.  Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.  Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyama-mwitu, wakatawanyika.  Kondoo zangu walitanga-tanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewauliza, wala kuwatafuta.  Basi, enyi wachungaji, lisikieni neon la BWANA;  Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo zangu; kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la BWANA;  Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo zangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo zangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao”. 
Warumi 16:17-18; Wafilipi 3:18-19; Yeremia 23:10-36
Baada ya hapo ujumbe mwingine ulishuka na kulilenga Kanisa la KLPT Mbezi Luis ukisema:
“Nimewachagua ninyi Kanisa la Mbezi Louis, ninawatuma kutangaza MSAMAHA, waambieni watu Bwana ameisamehe Tanzania, na haya mambo ya uchomaji wa makanisa hayatakuwepo tena, lakini msipogeuka nitawaangamiza kwa upanga Asema Bwana wa Majeshi”.
Amosi 3:6 “Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope?  Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?”.  Isaya 1:19-20
Alisema tusipogeuka hatakuja tena kwa njia ya kuchoma makanisa, bali kwa njia anayoijua yeye.


0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA