Friday, May 09, 2014
0
Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya viongozi wanaozozana nchini Sudan Kusini, Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, yanatarajiwa kuanza tena mjini Addis Ababa Ethiopia.
Marekani inasema kuwa haina matumaini kuwa mazungumzo ya leo yataweza kuleta mafanikio yoyote.
Mgogoro huo wa kisiasa umesababisha maelfu ya watu kufariki huku zaidi ya wengine milioni moja wakiachwa bila makao.
Katika ripoti yake hapo jana, Umoja wa Matifa ulituhumu pande zinazozana kwa kufanya vitendo vya kukiuka haki za binadamu ikiwemo mauaji, ubakaji, kuwafanya wanawake kuwa watumwa wa ngono, kufanya mauaji ya halaiki na kuwabaka wanawake,.
Ripoti hiyo ilisema kuwa vitendo vingi vya uhalifu vilifanywa katika nyumba za watu, hospitali, misikiti , makanisani na katika makao ya umoja wa Mataifa ambako wakimbizi walikuwa wamekimbilia usalama wao.
Umoja wa Mataifa umetuhumu upande wa Rais Kiir na ule wa Machar kwa kukiuka haki za binadamu
Kadhalika ripoti hiyo imesema kuwa takriban watu milioni 5 wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Mkataba wa amani ulifikiwa kati ya Rais Kiir na Machar mnamo mwezi Januari lakini haukusitisha mapigano.
Wapatanishi nchini Ethiopia, wamethibitisha kuwa bwana Machar aliwasili Alhamisi kwa mazungumzo hayo mjini Addis Ababa.
Mazungumzo ya leo yatalenga kumaliza vita na kusuluhisha tatizo la kugawana mamlaka.
Mawaziri wa serikali wamesema kuwa kile ambacho serikali inakipa kipaombele ni kusitisha vita na kujadili swala la kipindi cha mpito.
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya nje Barnaba Marial Benjamin, alinukuliwa akisema kuwa swala la serikali ya mpito halitajadiliwa na kuwa Rais Kiir ataendelea kuwa Rais hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA