Monday, May 12, 2014
0
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana.
Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata ushauri nasaha.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa mpenzi wake wakati huo,Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA