Saturday, May 10, 2014
0
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesikitishwa na hatua ya kutekwa nyara kwa zaidi ya wasichana 200 wa shule nchini Nigeria na kundi la wanamgambo wa kiislamu la boko haram.
Baraza hilo pia limeshtumu mashambulizi ya hivi karibuni ya kundi hilo,huku likitaka wale wanaotekeleza vitendo kama hivyo kukamatwa mbali na kuwekewa vikwazo.
Wataalam wa Marekani,Uingereza na Ufaransa wamewasili nchini Nigeria ili kusaidia kuwatafuta wasichana hao.
Marekani na Uingereza zinasema kuwa zitalipatia kipaumbele ombi la Nigeria la kutuma ndege za upelelezi.
Wakati huohuo Katika tukio ambalo si la kawaida, mke wa rais wa Marekani Michelle Obama anatarajiwa kutoa taarifa ya kila juma ya mumewe itakayoangazia utekaji nyara wa wasichana wa shule nchini Nigeria.
Wake wa marais kwa kawaida hukataa kujihusisha na sera za kigeni ,lakini bi. Obama amekuwa mkosoaji mkubwa wa kundi la wanamagambo wa kiislamu ambao waliwateka nyara wasichana hao.
Awali bi Obama aliweka picha katika mtandao wa tweeter ilio na maneno yanayosema 'Warudisheni wasichana wetu'.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA