Sunday, May 04, 2014
0
Watu kadhaa wamehofiwa kufariki na wengine kujeruhiwa kufuatia milipuko miwili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi ambayo imelenga mabasi mawili ya abiria.
Mabasi hayo yalilipuliwa katika eneo la barabara ya Thika karibu na mji mkuu.
Mlipuko mmoja umetoa katika basi la abiria ambalo lilikua likisafirisha abiria kutoka mjini Nairobi katika barabara ya Thika ambayo kawaida ina shughuli nyingi.
Basi la pili lililipuliwa karibu na hoteli moja iliyo umbali wa dakika chache kutoka jengo kubwa zaidi la maduka katika katika eneo hilo.
Shughuli za uokoaji zinaendelea na bado hakuna taarifa rasmi kuhusiana na watu waliouawa au kujeruhiwa kwa jumla. Picha za televisheni zinaonyesha mabasi hayo yakiwa yameharibiwa na madirisha kuvunjika.
Ni hapo jana tu ambapo watu wanne waliuawa na wengine wapatao ishirini kujeruhiwa katika shambulio lingine ambapo grunedi ilirushwa katika kituo cha mabasi ya abiria.
Shambulio la pili lilitokea karibu na mkahawa mmoja maarufu lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Mashambulio haya yanatokea mwezi mmoja tu baada ya serikali kuanzisha oparesheni ya usalama baada ya kukumbwa na mashambulio mengine hapo awali na pia kupata vitisho kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Alshabab waliodai kutekeleza shambulio la Westgate ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA