Friday, May 09, 2014
0
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anasema Marekani itafanya kila iwezalo ili kufanikisha kuachiwa huru kwa wasichana 276 waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram.
Akizungumza Alhamisi mjini Washington Kerry alisema kikosi cha washauri wa kijeshi cha Marekani kinawasili Nigeria ili kusaidia masuala ya mawasiliano , usafiri na ujasusi.

“Timu yetu hivi sasa inawasili Nigeria na watafanya kazi kwa karibu na serikali ya  rais wa Nigeria Goodluck Jonatahan  kufanya kila tuwezalo kuwarudisha wasichana hao kwa familia zao na jumuiya zao. Tutafanya kila tuwezalo kupambana na ubaya wa Boko haram”. Alisema
Nchi nyingine zisizopungua tatu zimeahidi kuisaidia Nigeria katika utafutaji huo. Uingereza imeahidi kutoa msaada wa satellite wakati Ufaransa imesema itasaidia kutuma askari.

Akizungumza kwenye mkutano wa uchumi wa dunia alhamisi huko Abuja Nigeria Rais Goodluck  Jonathan aliishukuru China , ikiwa ni nchi iliyojitokeza hivi karibuni na kuahidi  kutoa msaada wa utafutaji wasichana hao.
Kiongozi wa Boko Haram amesema ana nia ya  kuwauza wasichana hao ambao walitekwa nyara kutoka kwenye shule moja huko katika jimbo la Borno Nigeria April 14.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA