Wednesday, May 28, 2014
0
Huduma za simu iitwayo Silver line iliyoanzishwa kusaidia wazee wanaokumbwa na upweke huko Uingereza imepokea idadi kubwa ya wapigaji simu.
Zaidi ya simu mia elfu zimepokelewa katika kipindi cha miezi sita tangu huduma hiyo kuanzishwa.
Bi Esther Rantzen mwanzilishi wa huduma hiyo Silver Line, anasema kiwango hicho kikubwa cha wapigaji simu ni dhihirisho halisi la tatizo la upweke linalokumba wengi wa wazee katika mfumo wa kisasa wa maisha nchini Uingereza.
Mfumo wa kisasa wa maisha wa Uingereza walaumiwa kuchangia upweke unaokumba wazee.
Wengi wa wazee hao waliopiga simu huelezea jinsi wanavyoishi peke yao na mara nyingi hukosa hata mtu wa kuzugumza nao tu ndiposa hupiga simu laini hiyo kutafuta angalau sikio la kuwasikiliza.
Nusu wa waliopiga simu wamesema wanaeza kukaa kutwa bila kuzungumza na mtu , ilhali mmoja kati ya kumi wakasema huchukua hata zaidi ya wiki nzima bila kupata mtu wa kuzungumza nao.
Utafiti wa kisaikolojia wasema upweke mwingi unaeza kuleta madhara kama vile majonzi, msongo wa mawazo na athari nyenginezo za kiafya na hasa kiakili.
Tahadhari imetolewa kwa nchi zinazoendelea hasa barani Afrika kufanya jitihada kuzuia mmomonyoko wa kimaadili na utamaduni wa kutunza wazee ili kuepukana na hali kama hiyo.


0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA