Thursday, July 17, 2014
0

Je ni kweli wake wanaponenepa upita kiasi ndio sababu ya waume zao kuwa na mipango ya kando?
Nchini Kenya mjadala umezuka kwenye mitandao ya kijamii kufuatia maandishi ya mwanamke mmoja akiwalaumu wanawake wanene kupita kiasi kwa masaibu yanayowakumba katika ndoa zao.
Njoki Chege aliandika katika gazeti la Daily Nation Jumapili na kwenye blogu yake kusema kuwa sababu ya wanaume waliooa kuwa na mipango mingi ya kando ni wake zao kujisahau na kuwa wanene kupita kiasi.
Amesema wanawake wanapoolewa na kubarikiwa na watoto , unene huzuka na hapa ndipo Njoki anasema pindi mwanamke anapoonza kunenepa na kuwa mzito kupita kiasi, waume zao husasau yule kidosho aliyemfumba macho hata akamuoa.
Anaongeza kusema wanawake hao huzua kila sababu kutofanya mazoezi na wakisema wana shughuli nyingi.
Njoki anasema bora wanawake waendelee kuwa na umbo mdogo ndipo wawapendeze waume wao
Kadhalika anasema wanawake hujipatia majukumu mengi na kujishughulisha kiasi cha kujisahahu. Wao husema unene umetokana na kupata mtoto lakini kwa Njoki, hicho ni kisingizio tu.
Waume zao wanapotupa jicho huku na kule na kujionea wasichana walio na umbo zuri basi huingia kwenye mtego wa kujiingiza katika zinaa.
Matamshi ya Njoki yamewakera wengi hasa wanawake na kuzua hisia mseto miongoni mwa watu wengi. Bila shaka aliandika maoni yake na sisi tunakuuliza tu maoni yako.
Kwa nini swala hili la unene na wembamba ndilo linatumiwa kama kigezo kwa wanaume waliooa kwenda nje ya ndoa?
Je unahisi kama kuna ukweli hapa au Njoki ana matatizo yake mwenyewe? Yeye mwenyewe ni mwembamba.
Blogu ya Njoki: Bofya http://goo.gl/POzgDi

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA