Wednesday, May 14, 2014
0
Wabunge nchini Uganda wamepitisha mswaada unaotoa adhabu kali kwa watu wanaowaambukiza wengine virusi vya HIV kwa maksudi.
Mswada huo unapendekeza adhabu ya kifungo cha hadi miaka 10 kwa wale wanaopatikana na hatia na pia inapendekeza wanawake wajawazito na wapenzi wao kupimwa virusi vya HIV.
Mbunge mmoja kwa jina Peter Aleper aliambia vyombo vya habari kuwa watu wanaowaambukiza wenzao virusi vya HIV kwa maksudi ni hatari kwa jamii.
"ni lazima waadhibiwe vikali kwa sababu kumuambukiza mtu HIV wakati unafahamu vyema kuwa wewe ni mwathiriwa ni uuhalifu,'' alisema mbunge huyo. Ni hatari sana kwa sababu mru huyo anaweza kuichanganya jamii na kumaliza watu.''
Lakini wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na mashirika ya kutetea haki za wanyonge, wamepinga vikali mswada huo, wakisema kwamba haitafanya lolote kudhibiti ongezeko la visa vya maambukizi.
Wengi wanasema kuwa mswada huo utaongeza tu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo. Pia wanasema kuwa watu watahofia kupimwa kwa hofu ya kutengwa na jamii.
Mswada wenyewe umepitishwa baada ya sheria kali inayopinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kupitishwa na rais Yoweri Museveni mwezi Februari.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA