Friday, May 16, 2014
0
Makumbusho mapya  yanayoeleza yale yaliyotokea wakati wa mashambulizi ya Septemba 11 litafunguliwa kwa watu wote wiki ijayo baada ya kufunguliwa na Rais Barack Obama siku ya Alhamisi May 15 2014.
Rais wa Marekani Barack Obama  amesema makumbusho hayo yanatarajiwa  kufunguliwa kwa umma wiki ijayo.

Makumbusho hayo yaliyogharimu  dola milioni 700 na mnara wa kumbu kumbu yamejengwa kwa miaka kadhaa .  Ukamilishaji wake siku zote umekumbwa na mizozo juu ya ujenzi wake, kuchelewesha kazi na mpaka leo kama ikiwa mabaki ya miili ya wale wasiotambuliwa  yazikwe chini ya jengo hilo au juu.

Makumbusho hayo yako karibu na chini  ya ardhi yakienda mpaka kwenye eneo la vyuma ambalo kuliwekwa jengo la World Trade Centre. Vyuma vikubwa vilivyotoka kwenye jengo lililoharibiwa vinaonyeshwa  pamoja na vitu mbali mbali vya makumbusho ya mashambulizi hayo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA