Wednesday, May 14, 2014
0
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji ya mwanahabari raia wa Ufaransa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Baraza hilo limesema kuwa kifo cha mwanahabari huyo ambaye pia alikuwa mpiga picha, aliyekuwa na umri wa miaka 26 , lazima kichunguzwe na wale waliohusika wachukuliwe hatua.
Rais wa Ufaransa amesema kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuwapata wauaji.
Duru zinaarifu kuwa mwili wake ulipatikana pamoja na maiti wengine wanne katika lori lililokuwa linaendeshwa na wapiganaji wa kiisilamu katika eneo la Magharibi mwa nchi la Bouar.
Watu kumi wamezuiliwa na polisi ili kuhojiwa

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA