Wednesday, May 07, 2014
0
Tume huru ya uchaguzi nchini Africa Kusini-IEC imejiandaa vyema kufanya uchaguzi wa kitaifa na wa majimbo unaofanyika Jumatano, Mei 7.
Ikitajwa kama aina maalum  ya kura, wapigaji kura ambao ni wagonjwa, maafisa wa usalama  na maafisa wa uchaguzi ambao watakuwa wakifanya kazi siku ya uchaguzi  waliruhusiwa kupiga kura mapema kabla ya uchaguzi.

 Msemaji wa tume huru ya uchaguzi ya Afrika kusini, Kate Bapela, anasema “Waafrika kusini ambao wamepiga kura ngambo na mbele ya mipaka ya Afrika kusini wameshamaliza kupiga kura na tumefurahi na maendeleo. Tayari kura zilizopigwa zinaletwa nchini kuweza kuhesabiwa na kura zitakazo pigwa siku ya uchaguzi hii leo Mei 7”.

Bi. Bapela anasema hatua zimechukuliwa kuhakikisha kusadikika kwa kura hizo.  “Tuko tayari kabisa, kwa sababu tufikapo katika kituo cha matokeo, ni ishara bayana kwamba tuko tayari kuendelea na uchaguzi. Maafisa wetu wametayarishwa, mfumo wa kutowa matokeo uko tayari kuweka matokeo kadri yanavyotokea katika vituo vya upigaji kura kote nchini”.


Matokeo ya kura kutoka vituo vya uchaguzi kote nchini yatahesabiwa katika makao makuu ya IEC ili kutathmini matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Afrika kusini, IEC inaweza kutangaza matokeo ya uchaguzi katika kipindi cha siku saba baada ya kuhitimishwa kupigwa kura.
Bi Bapela anasema anadhani ifikapo Ijumaa matokeo mengi yatakuwa yamefika  na iwapo kila kitu kitakuwa sawa  basi lazima tutangaze matokeo mwishoni mwa wiki ijayo. Anasema haya yote yanategemea uwezo wa maafisa wetu kuweza kuweka matokeo na kuhakikisha kila kitu kimefanywa ipasavyo. Anasema maafisa wa tume ya uchaguzi wamepatiwa mafunzo ya kutosha ya kuandaa uchaguzi na kuahidi kufanya uchaguzi uliowazi.

Anasema anatumai watapata si chini ya asilimia 70 ya wapigaji kura  na wanataraji kwamaba wa- Afrika kusini watajitokeza kwa idadi kubwa na kutumia fursa hii kadhalika kusheherekea miaka 20 ya demokrasia.

Takwimu za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kwamba chama tawala cha Africa National Congress-ANC kitashinda uchaguzi  licha ya ushindani  mkali kutoka kwa vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja na chama cha Democratic Alliance-DA.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA