Friday, July 11, 2014
0

Watu waliojihami wamevamia kijiji cha Pandanguo katika Kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya.
Chifu wa eneo hilo Karisa Charo Karisa, anasema kuwa shule na nyumba nne ziliteketezwa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa usiku wa kuamkia leo.
Duru zinaarifu kuwa washambuliaji hao waliiba bunduki kutoka kwa watu polisi wa dharura na kufanya mashambulizi hayo.
Kwa sasa hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi wa mashambulizi hayo.
Duru zinasema kuwa washambuliaji hao waliiba bunduki sita kutoka kwa polisi wa dharura kabla ya kuteketeza nyumba.
Kwa sasa hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi.
Inaarifiwa kuwa wanajeshi wamepelekwa katika eneo hilo kudhibiti usalama.
Mnamo mwezi Juni watu watano waliuawa katika eneo hilo la Pandanguo ambalo liko umbali wa kilomita 30 kutoka Mpeketoni ambako mashambulizi mengine yaliwaacha watu zaidi ya sitini wakiwa wameuawa.
Waathiriwa wengi wa mauaji walipatwa wakiwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo na koo zao zikiwa zimekatwa.
Eneo la Lamu ambao liko Pwani ya Kenya limekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara tangu mwezi Juni huku watu wakiuawa kwa misingi ambayo bado ni tata.
Mashambulizi ya Kwanza yaliyofanyika mjini Mpeketoni, yalisemekana kufanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab ingawa serikali alilalaumu wanasiasa kuyachochea mashambulizi hayo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA