Watu wawili wamekamatwa na
Polisi wakihusishwa na shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa
'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.
Shambulizi hilo liliyokea siku ya jumatatu saa nne usiku.Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
0 comments:
Post a Comment