Thursday, April 24, 2014
0
Mlinzi mmoja nchini Afghanistan amewaua kwa kuwapiga risasi madaktari 3 raia wa Marekani wanaofanya kazi katika hospitali moja mjini Kabul.
Hosptali hiyo inayowahudumia watoto na kutoa huduma za afya ya uzazi inasimiwa na shirika la kikirsto la Marekani CURE.
Madaktari wengine wawili pia walijeruhiwa.
Mlinzi huyo kisha alijipiga risai na kwa sasa anazuiliwa na polisi.
Hili ndilo shambulizi la pili linalowalenga wakristo nchini Afghanistan mwaka huu.
Mwezi Machi wanamgambo wa Taliban walivamia jumba moja la kulala ambalo hutumiwa na raia wa kigeni wananaofanya kazi na shirika moja la kilimo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA