Saturday, April 05, 2014
0
 Paris inapata meya wake wa kwanza mwanamke lakini chama chake tawala cha Socialistics kilipata kipigo katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Ufaransa. Anne Hidalgo mzaliwa wa Spain alimshinda mpinzani wake m-conservative kushinda wadhifa wa cheo cha juu katika mji mkuu wa Ufaransa. Hidalgo awali alihudumu kama naibu wa meya anayemaliza muda wake, Betrand Delanoe. Alishinda kwa ahadi ya kujenga nyumba mpya za umma na....
kurahisisha zaidi mfumo wa huduma ya kulea watoto kwa familia za Paris.
Waangalizi wengi wa kisiasa wanaiangalia ofisi ya meya wa Paris kama hatua moja kusonga mbele kwa urais wa Ufaransa.

Lakini chama cha Hilalgo cha Socialists hakikufanya vyema katika miji na miji mikubwa mingi mingine ya Ufaransa,  imepoteza uungaji mkono kwa wanaopinga uhamiaji na wanaopinga chama cha European Union national Front.

Uchaguzi unaonekana kama kura ya maoni kwa rais asiye maarufu, Francois Hollande.
Wapiga kura wamekasirishwa na kudorora kwa uchumi na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira.



0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA