Tuesday, April 15, 2014
0
Rais wa Uganda Yoweri Museveni,amemkabidhi mfalme wa Buganda mali ambayo ufalme huo ulipokonywa mnamo miaka ya sitini.
Mali hiyo ambayo ni pamoja na ardhi, majumba na hati za kumiliki ardhi ilikabidhiwa kwa mflame wa Buganda katika sherehe iliyofanywa mjini Kampala.
Buganda ndio ufamle mkubwa wa kitamaduni uliosalia nchini humo. Ulifutiliwa mbali na aliyekuwa Rais Milton Obote mwaka 1966 lakini ukarejeshwa tena na Rais Museveni mapema miaka ya tisini.
Rais Museveni alikabidhi nyaraka za umiliki wa mali hiyo kwa naibu mkuu wa Katikiro au waziri mkuu wa ufalme huo Emmanuel Sendaula katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Rais mjini Entebbe.
Kadhalika Rais Museveni alisifu ushirikiano uliopo kati ya....
utawala wa Kabaka na serikali.
Museveni aliongeza kuwa uhusiano kati ya pande hizo mbili utasalia kuwa mzuri na kwamba vizingiti vilivyokuwepo vimeondolewa na kuwa Rais hataki mzozo wa kijamii.
Alisema Kabaka Ronald Mutebi wa pili, anaweza kuzuru Kayunga bila wasiwasi wowote.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA