Monday, April 07, 2014
0



Wezi wa mifugo weanaoshukiwa kuwa "Wafulani" wamewaua watu 79 katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Nigeria katika jimbo la Zamfara. Vyombo vya habari nchini Nigeria mnamo Jumapili vilimtaja Msemaji wa Gavana wa jimbo hilo, Bwana Nuhu Salihu Anka, akisema kuwa watu hao waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa mifugo kutoka jamii ya Fulani, ambao ni wachungaji.
Maafisa wakuu katika Serikali ya jimbo la Zamfara walihudhuria mazishi ya watu hao 79 katika eneo hilo hiyo jana. Naye msemaji wa polisi wa Taifa, Lawal Abdullahi alisema kuwa watu 30 waliuawa katika shambulio la Jumamosi wakati wachungaji waliokuwa na bunduki kutoka jamii ya Fulani walipovamia mkutano wa wajumbe kutoka Majimbo ya Zamfara, Kaduna, Kebbi na Kastine wakijadiliana changa moto za....
usalama katika maeneo yao.
Anka anatajwa kusema kwamba wamekuwa wakikabiliana na mashambulizi mabaya sana ya magenge ya watu wenye silaha na wezi wa ngombe lakini shambulio hili la sasa ndiyo baya zaidi.
Kiongozi mmoja wa kijadi amenukuliwa akisema idadi ya waliokufa ni wengi zaidi. Alisema hadi kufikia Jumapili walikuwa wamewazika watu 120 kutokana na shambulizi hilo na kuwa idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka zaidi.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA