Wednesday, April 02, 2014
0

Hali ya wasi wasi imetanda nchini Chile baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi.
Viongozi nchini Chile wameamuru kuhamishwa kwa watu kutoka pwani ya kaskazini mwa taifa hilo baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi.
Tetemeko hilo linalofikia kiwango cha 8.2 katika vipimo vya Rikta, limeibua tahadhari ya janga la Tsunami katika eneo zima la Kusini Marekani.
Taasisi ya maswala ya Ardhi ya marekani imearifu kuwa kitovu cha tetemeko hilo ilikuwa takriban kilomita 84 pekee kutoka kwenye ukanda wa bahari na kilomita kumi pekee ndani ya ardhi.
Barabara kuu ya Iquique, mji ulioko karibu sana na kitovu cha tetemeko hilo, ardhi imepasukapasuka huku watu wakijaribu kukimbia kutoka eneo ilikotokea tetemeko hilo kubwa zaidi kutokea mwaka huu.
Viongozi Nchini Chile wanasema kuwa...
kumekuwepo na maporomoko ya ardhi, huku majumba katika nchi jirani ya Peru na Bolivia yakitetemeshwa.
Mawimbi yenye kimo cha mita mbili tayari yamefika ufukweni takriban dakika 45 pekee tangu tetemeko hilo kutokea.
Tahadhari ya Tsunami imetolewa katika mataifa yote ya Latin Amerika hasa katika maeneo ya pwani ya bahari ya Pacific.
Mwezi uliopita, zaidi ya watu elfu moja waliondolewa makwao kutoka katika maeneo yayo hayo, baada ya tetemeko lililofikia kipimo cha 6.7 katika viwango vya Rikta kutokea.
Chile ni moja kati ya mataifa yanayoathirika kwa kiwango kikubwa na matetemeko ya ardhi..
Mwaka wa 2010 maeneo ya katikati na kusini mwa taifa hilo yaliathirika pakubwa na tetemeko lililotikisa ardhi kwa kima cha 8.8 kwenye vipimo vya rikta na kutibua tsunami.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA