Wednesday, April 16, 2014
0
Kiongozi wa jimbo lenye idadi kubwa ya watu nchini Australia,New South Wales, amejiuzulu baada ya kukosa kutangaza kuwa alipata zawadi ya mvinyo yenye thamani ya dola 2,800.
Waziri mkuu wa New South Wales ,Barry O'Farrell alikiri kuwa alisahau au alighafilika kwa bahati mbaya baada ya kuambia jopo moja linalochunguza visa vya ufisadi kuwa hakuwahi kupokea mvinyo wowote kutoka kwa mtu yeyote.
Bwana O'Farrell, alisema hangeweza kukumbuka kumpigia simu mfanyabiashara Nick Di Girolamo, aliyemkabidhi zawadi ya mvinyo mwaka 2011.

'hakukumbuka kamwe '

O'Farrell, ambaye ni kiongozi wa chama cha Liberal, katika jimbo la New South Wales, alitangaza kujiuzulu mjini Sydney Jumatano.
Aliambia wandishi wa habari kwamba....
haikuwa nia yake kulipotosha jopo hilo.
"nakubali kuwa kuna ujumbe wa shukrani nilioutia saini na kama mtu ambaye anaamini katika uwajibikaji, ninakiri makosa yangu, '' alisema O'Farrell.
Aliongeza kuwa waziri mkuu mpya wa jimbo hilo atachaguliwa katika kikao cha bunge wiki ijayo.
"siwezi kueleza kwa kweli ikiwa ilikuwa zawadi na nilivyoipata,'' alisema waziri mkuu huyo.''Lakini nakiri kosa langu.''
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott, amesema kuwa kujiuzulu kwa bwana O'Farrell, ilikuwa ishara ya maadili mema wala sio ufisadi. Amemtetea akisema kuwa alighafilika kweli wala hakunuia kusema uongo kwa maksudi

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA