Tuesday, April 15, 2014
0
Mahakama ya juu zaidi nchini India imetoa uamuzi wa kihistoria unaotambua watu waliobadilisha jinsia yao kama watu wa kawaida katika jamii.
Kawaida kuna jinsia mbili, mke au mume lakini mahakama hiyo imesema kuwa watu wanaoamua kubadilisha jinsia yao kuambatana na hisia zao pia ni lazima watambuliwe na jamii.
Mfano wa watu kama hao ni mtu anayezaliwa kama mwanamke lakini anahisi kisaokolojia kuwa yeye ni mwanaume na hivyo hubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamume kwa hata kufanyiwa upasuaji.
Uamuzi huu wa mahakama bila shaka ni wa.....
kihistoria

"ni haki ya kila binadamu, kuchagua jinsia wanayoitaka,'' alisema jaji katika uamuzi huo ambao unawapa watu hao haki ya kujitambulisha kama wanaume au wanawake

Iliamuru serikali kuwapa watu hao nafasi za kazi na elimu kama jamii ya watu waliotengwa. Mahakama pia imeitaka serikali kuwapa huduma muhimu watu hao wanaochagua kujitambulisha watakavyo.
Takwimu zinasema kuwa watu milioni mbili nchini India wamebadilisha jinsia yao.
Wanaharakati wanasema kwamba, watu hao wanatengwa na kuishi katika umaskini mkubwa na pia wanachukiwa kwa sababu ya kubadilisha jinsia yao.
Wengi hujikimu kimaisha kwa kuwa waimbaji , kuombaomba barabarani na kujihusisha na biashara ya ngono.
Kadhalika wanaharakati wanasema kuwa watu hao hunyimwa huduma za matibabu hospitalini.
''Watu hawa ni raia wa India na lazima waheshimiwe na kupewa nafasi ya kunawiri maishani,'' alisema jaji katika uamuzi wake.
"lengo la katiba ni kuhakikisha kila mtu wa India anapewa nafasi ya kuishi vyema na kujiendeleza maishani, licha ya jinsia , dini na jamii anakotoka''

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA