Sunday, March 23, 2014
0
Wakati Dunia ikiwa bado inajiuliza maswali mengi kuhusiana na ilipo ndege ya Malaysia ambayo imepotea kwa zaidi ya wiki tatu sasa. Wanasayansi nchini Ufaransa wamebaini kwamba virusi vya Ugonjwa wa Ebola ndio chanzo cha ugonjwa wa homa ya haemorajic nchini Guinea ambayo inaaminika kuwauwa karibia watu sitini.
Ugonjwa huo ambao unaweza kuambukizwa kwa haraka ulianza nchini humo yapata...
majuma sita yaliopita.
Dalili za ugonjwa huo ni kutoka damu,kuharisha pamoja na kutapika.
Afisa mmoja wa wizara ya afya nchini Guinea amesema kuwa takriban visa vinane vya ugonjwa huo vimeripotiwa hususan kusini mwa taifa hilo.
Amsema kuwa serikali ya taifa hilo inatumia kila njia kukabiliana na ugonjwa huo lakini inaendelea kushindwa.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa Ebola ambao husambazwa kupitia kugusana na walioambukizwa.
BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA