Maafisa watatu kutoka katika idara ya kumlinda Rais
wa Marekani Barack Obama katika ziara yake nchini Uholanzi, wamerejeshwa
nyumbani kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Jarida la Washington Post nchini Marekani
limeripoti kwamba mmoja wa askari hao alikutwa akiwa mlevi chakari
kiasi cha kupoteza fahamu katika hoteli moja mjini Amsterdam.
Mapema Jumapili, siku moja kabla ya
Obama kuwasili nchini humo, wafanyakazi wa...
hoteli waliarifu ubalozi wa
Marekani nchini Uholanzi kuhusu walivyompata askari huyo katika hali ya
kutojitambua.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa
kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo, ingawa alisisitiza kuwa watatu
hao wameachishwa kazi kwa muda uchunguzi ukiendelea.
Tukio hilo lilitokea kabla ya Rais Obama kuwasili Uholanzi kwa mkutano kuhusu kawi ya Nuklear.
Shirika hilo la ujasusi limekuwa likijaribu kujisafishia sifa yake hasa baada ya kukumbwa na kashfa mbali mbali.
Mnamo mwaka 2013, majasusi wawili waliondolewa
katika kikosi cha ulinzi cha Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na
kashfa ya ngono na utovu wa nidhamu.
Na mnamo mwaka 2012, majasusi kadhaa
waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini
Cartagena, Colombia.
SOURCE:BBC SWAHILI |
0 comments:
Post a Comment