Friday, March 14, 2014
0
NAJUA WAJUA NAMI NAKUJUZA WEWE UNAYETAKA KUJUA MENGI YA DUNIA..Kuna band inayoitwa "HATEBEAK" ambayo mwimbaji kiingozi wake ni Kasuku, ambaye anauwezo mkubwa wa kuimba. Acha ubishi haya mambo yapo Duniani. Lakini pia.... huko Japan kuna kituko kingine cha mwaka kimetokea ambapo jamaa ameishi na mwanamke kwa zaidi ya mwaka nyumbani kwake bila ya yeye mwenyewe kufahamu.. Jamaa alistuka baada ya kuona "stock" yake ya chakula ikipungua kwa kasi wakati yeye anaishi peke yake, hivyo akaamua kuweka Camera ili kubaini hicho "kidudu mtu" kinachomuibia msosi wake, na hapo ndipo Mama huyo mwenye umri wa miaka zaidi ya 54, alipofumwa akiwa amejificha kwenye Kabati la nguo.. Khatariii

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA