Thursday, March 06, 2014
0
Bungeni ni sehemu ambayo inakutanisha watu tofauti wenye uwezo na kaliba zenye kutofautiana, kuanzia Elimu, Fedha, Makuzi, Imani na hata....
Uwezo wa kuchanganua mambo na utendaji pia. Si Bungeni tu, lakini mchanganyiko wa watu kama huo unapokutana mahali popote zinahitajika BUSARA, HEKIMA na UVUMILIVU wa hali ya juu kwa kila mmoja, ili kuweza KUVUMILIANA, KUSTAHIMILIANA, KUPENDANA, KUHESHIMIANA na hata SUBIRA kwa kila mmoja aliyepo katika HADHIRA hiyo..
Na haya yote yatawezekena tu ikiwa kila mmoja wetu kwa IMANI yake kumuomba MUNGU ili kuwezesha yooote hayo kwa wajumbe wetu wa Bunge la KATIBA..
Tuliombee Bunge letu ndugu zangu, Tuliombee Taifa letu wapendwa.. huko kwingineko kulikotokea machafuko mambo yalianza kuharibika kidoggo kidogo kabla ya kupelekea hali kuwa mbaya zaidi. 
IPENDE TANZANIA, anza kuomba sasa ili tuvuke kipindi hiki kigumu kwa TAIFA letu.. 
Much love.. PAMOJA TUNAWEZA!!

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA