Wednesday, March 26, 2014
0
Maelfu ya watoto nchini Uingereza na Wales, wanakabiliwa na tisho la kukosa elimu huku walimu wao wakigoma.
Walimu hao wanagoma wakitaka nyongeza ya mishahara, malipo mazuri ya uzeeni na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.
Wanachama wa chama cha walimu, (NUT) watashiriki katika mgomo huo huku wakiacha shule nyingi bila....
walimu huku masomo yakisitishwa.
Walimu hao wamesema hawakuwa na budi ila kuondoka kazini kwani hakuna suluhu la matatizo yao.
Wizara ya elimu hata hivyo imelalamika ikisema kuwa mgomo huo unaathiri maisha ya wazazi na elimu kwa watoto.
Mgomo huu ulianza baada ya walimu kukubaliana kupiga kwa kura mwezi Mei 2011 na Juni 2012.
Asilimia 92 ya walimu walipiga kura ya ndio kwa gomo kufanyika.
Chama cha walimu nchini humo kimekuwa kikivutana na serikali kwa miaka miwili sasa na hata kufanya migomo midogomidogo hadi mgomo huu mkubwa ukafikiwa.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA