Sunday, March 30, 2014
0
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri imesema kuwa inachunguza maneno yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii yakiwa na kitambulisho, yaani "hashtag", yanayomtusi waziri wa ulinzi aliyestaafu ili kugombea urais, Field Marshall Abd-el-Fattah el-Sisi.
"hashtag" hiyo ambayo tafsiri yake ni "mpigie kura kuwadi", imesambazwa kwenye Twitter zaidi ya mara 100-milioni na imependwa na watu zaidi ya 40,000 kwenye Facebook.
Inaarifiwa kuwa wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema itawakamata watu wanaoitumia....
sana heshtegi hiyo.
Maneno hayo piya yamekuwa yakichorwa kwenye kuta za mjini Cairo chini ya mabiramu ya picha za Bwana Sisi.
Field Marshall E-Sisi aliipindua serikali iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasi ya Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood mwezi Julai mwaka jana.
Raisi Morsi wakati huo Akimuapisha Eli-sisi kuwa waziri wa Ulinzi..

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA