Monday, March 17, 2014
0
Walevi nchini Kenya wamekuwa wakilalamika kuhusu matumizi ya kifaa malum cha kupima kiwango cha pombe walichokunywa madereva wa usiku wanapokuwa wakiendesha magari wakiwa walevi.
Sheria ya kulewa na kuendesha magari nyakati za usiku imekuwa kali kwani...
polisi wanasisitiza kuwa lazima madereva wa usiku wapimwe ikiwa wamekunywa pombe kupita kiasi hali inayotishia usalama wao barabarani.
Tangu kifaa cha ''Alco-Blow'' au kifaa kinachotumiwa kupima kiwango cha pombe alichokunywa dereva kuanza kutumika kama njia ya kudhibiti ulevi barabarani mezi kadhaa iliyopita, utata umeibuka kuhusu usalama wa kukitumia kiafya kwani kinatumiwa na madereva wengi.
Lakini polisi wamesema kuwa watu wasiwe na wasiwasi kwani tahadhari zote zimechukuliwa ili kuzuia tisho lolote la afya kwa watumiaji.
Na pia sio lazima uweke mdomo wako kwenye kifaa bali unapuliza tu na kinachukua vipimo.

Usalama barabarani

Usalama barabarani umekuwa tatizo kuu nchini Kenya ambapo takriban watu elfu tatu hufa kutokana na ajali za barabarani kila mwaka .
Idara ya trafiki imesema kuwa asilimia 85 ya ajali hizo husabishwa na makosa ya kibinadamu yanayochangiwa kakubwa na ulevi kupindukia.
Walevi wamepata afueni kwani kuna huduma ya usafiri kwa basi unatolewa kwa wanasalia kwenye baa kujiburudisha
Hayo yote ni kwa mujibu wa sheria kali ya kunasa madereva walevi. Ni dhahiri kuwa kuendesha gari ukiwa mlevi ni hatari kubwa , lakini kuna wale ambao hawajafurahishwa na jinsi seriklai imetimiza sheria ya kunasa madereva walevi.
Kumekuwa na mjadala mkali nchini Kenya ikiwa kifaa cha AlcoBlow ni salama au la kutokana na watu zaidi ya mmoja kukitumia wakati polisi wanapofanya ukaguzi wao katika vizuizi vya barabarani

Ujanja wa walevi

Josephat Baraza ni meneja wa baa moja jijini Nairobi, anasema kuwa wakati operesheni ya kurejesha usalama barabarani ni muhimu, imeleta hasa kwa wauza mpombe na wanaomiliki mikahawa.
Lakini wamekuwa wajanja nao kwani wamezindua huduma ya kuajiri madereva wanaoendesha magari ya wateja wa baa yao na kuwarejesha nyumbani kwa njia salama baada ya kunywa pombe na kuendesha magari yo huku wakijozolea balaa.
Walevi wamejaribu juu chini kujinasua kutoka katika mtego wa polisi wanaoshika doria barabarani. mitandao wa jamii kama Facebook na Twitter kuonya wenzao kutopitia bara bara waliko polisi.
Licha ya hayo, Charles Keitany ambaye ni afisa mkuu anayesimamia usalama wa barabara kuu za Kenya anasema lazima wataendela na operesheni ya kuwanasa madereva walevi.
Si mara ya kwanza polisi wa Kenya kutumia kifaa vya kupima kiwango cha ulevi, kila mara hatua hii imepata pingamizi kali kutoka kwa umma ambao wamepeleka kesi mahakamani kutaka kifaa hicho kutohalalishwa.
Mahakama moja jijini Nairobi ilitupilia mbali kesi hiyo.
Kawa sasa kuna Wakenya ambao wananunua kifaa hicho kwa matumizi yao binafsi lakini mkuu wa polisi anyesimima barabra kuu za Kenya anashauri unaponunua kifaa cha kibinafsi lazima upate cheti cha kudhibitisha uhalali wake kutoka kwa shirika la kitaifa linalodhibiti ubora wa bidhaa.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA