Monday, March 31, 2014
0
Waziri mkuu Ehud Olmert akiwa na Raisi George Bush Jr.
 Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Olmert amepatikana na hatia ya kupokea hongo.
Mahakama moja ya Mji wa Tel Aviv alimpata na hatia kiongozi huyo wa zamani katika ksahfa iliyotokea wakati akiwa Meya wa mji huo mkuu.
Inaarifiwa hongo ilitolewa na kupokelewa katika uuzaji wa kipande cha ardhi ili kuharakisha ujenzi wa nyumba za kifahari.
Kadhalika Mahakama imesema kesi hiyo imefichua utawala uliokuwa fisadi na ambao uliendeleza ufisadi mkubwa katika.....
kipindi cha miaka mingi.
Sakata hiyo iliyojuliakana kama 'Holy Land' iliyohusisha kipande cha ardhi mjini Tel Aviv ilipelekea Bw. Olmert mwenye umri wa miaka 68 kujiuzulu kama Waziri MKuu mwaka 2008.
Hii ndio mara ya kwanza Waziri Mkuu wa Israel amepatikana na hatia ya Hongo. Duru zinasema kuwa hukumu hii huenda ikawa mwisho wa ndoto ya kisiasa ya bw. Olmert.
Kwa muda mrefu Olmert alikana kufanya makosa yoyote na pia tuhuma sawa na hii dhidi yake zilitupiliwa mbali na mahakama mbali mbali.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA