Thursday, March 13, 2014
0
 Mahakama kuu mjini Delhi India imesema kuwa hukumu ya kifo dhidi ya wanaume wanne waliopatikana na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja itasalia.
Kitendo cha genge hilo kulisababisha ghadhabu kubwa nchini....
India kuhusu dhudluma zinazotendewa wanawake
Mawakili wao wamesema kuwa watakata rufaa.
Wanaume hao walimbaka msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 kwa zamu huku wakimzungusha mjini humo kabla ya kutupa mwili wake kando ya barabara Disemba mwaka 2012.
Alifariki wiki mbili baadaye akipokea matibabu hospitalini.
Kutokana na ghadhabu ya watu wengi nchini humo, serikali ililazimika kubuni sheria kali, dhidi ya dhuluma za kingono na pia kuzindua mahakama maalum ya kusikiliza kesi za ubakaji kwa haraka.
Mahakama hiyo iliwahukumu wanaume hao mwezi Septemba mwaka jana ikisema kuwa kesi yao ilistahiki adhabu ya kifo.


0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA