Monday, March 10, 2014
0

Serikali ya Syria inadaiwa kutumia mbinu zisizofaa kuwanyima chakula, raia, wasio na hatia na ambao pia ni wakimbizi.
Shirika la kimataifa la Amnesty International linasema kuwa serikali inatumia njia ya kuwanyima chakula raia kama silaha dhidi ya.....
wakimbizi ambao wako katika kambi za wakimbizi na ambao wanahitaji msaada wa dharura.
Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi 128 wamefariki katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk mjini Damascus kutokana na kukosa chakula.
Shirika hilo linasema kuna hali ngumu ya kibinadamu inayowakabili wakimbizi hao.
Shirika la Amnesty linasema kuwa familia nyingi zimelazimika kutafuta chakula katika jaa za takataka na kuhatarisha maisha yao.
Kulikuwa na ripoti za mapigano mapya kuzuka karibu na kambi hiyo mapema wiki hii.
Mwandishi wa BBC Rami Ruhayem, anasema kuwa mapigano yalisitishwa kwa muda ili kuweza kuwafikishia chakula wakimbizi mjini Damascus
Kambi ya Yarmouk ambayo inawahifadhi wakimbizi 17,000 hadi 20,000 wa kipalestina na wengine raia wa Syria, imeshuhudia vita vikali mno katika siku za hivi karibuni.
Kambi yenyewe imekuwa bila stima(umeme)  tangu Aprili mwaka 2013 na nyingi ya hospitali za mji huo zimefungwa baada ya kukosa vifaa muhimu.
SOURCE BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA