Friday, March 28, 2014
0
 Hifadhi moja ya wanyamapori iliyowagadhabisha watu kwa kumuua Twiga nchini Denmark mwezi jana, imewaua Simba wanne ili kutoa nafasi kwa Simba mmoja mgeni anayetarajiwa kuletwa katika mbuga hiyo hivi karibuni
Wasimamizi wa hifadhi hiyo mjini Copenhagen, waliwaua Simba wawili wadogo na wawili wakubwa walio wazaa wadogo hao baada ya kukosa nafasi ya kuwahifadhi.
Hifadhi hiyo ilisema kuwa Simba hao wakubwa waliokuwa na miaka 16 na 14, walikuwa wamefikisha umri wa...
kupekwa mbugani.
Mwezi jana hifadhi hiyo ilimuua Twiga mkubwa mwenye afya tele kwa sababu alionekana kuwa na mahitaji mengi kuliko uwezo wa hifadhi hiyo.
Taarifa kutoka katika hifadhi hiyo ilisema kuwa kwa sababu Simba walikuwa wakubwa walihitaji kuuawa huku wadogo wakiuawa kwani hawana uwezo wa kujilisha bila ya wazazi wao.
Twiga aliyeuawa alikuwa kitoweo kwa Simba wengine katika hifadhi hiyo

Kulingana na wasimamizi, Simba huyo mgeni angeuawa na Simbawakubwa kwa sababu ndio kawaida ya wanyama hao kuua wale ambao hawajawaza.
Walisema kuwa walikuwa wametoa ombi kwa hifadhi zengine kumchukua Simba huyo mchanga lakini hakuna yeyote aliyekubali kufanya hivyo.
Simba huyo mgeni anapaswa kuwasili katika hifadhi hiyo katika siku chache zijazo na atakaribishwa na simba wawili wa kike waliozaliwa mwaka 2012 na ambao wako tayari kuzaa.
Mwezi jana mkuu wa hifadhi hiyo, alitishiwa maisha yake baada ya kumuua Twiga huyo ambaye baadaye alifanyiwa upasuaji mbele ya umati wa watu.
Watu duniani kote hasa wapenzi wa wanyama wa porini, walighadhabishwa mno na hatua ya kuuawa kwa Simba hao na Twiga.
Licha ya kilio cha wengi, mbuga hiyo ilisema kuwa haiko tayari kubadilisha taratibu zake za kazi.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA