Monday, March 31, 2014
0
 Mahakama moja nchini Pakistan imemsomea mashitaka ya uhaini mtawala wa zamani wa kijeshi Pervez Musharraf, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkuu wa majeshi nchini humo kushitakiwa.
Bwana Musharraf anatuhumiwa kusitisha katiba kinyume cha sheria na kutangaza utawala wa sheria mwaka 2007.
Amekana mashitaka na daima amedai kuwa mashitaka dhidi yake yana msukumo wa kisiasa. Atakabiliwa na adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.
Bwana Musharraf alikuwa rais wa Pakistan tangu mwaka...
2001 hadi 2008, alikuwa mmoja wa watawala wa Pakistan waliokaa madarakani kwa muda mrefu.
Alikwenda kuishi uhamishoni mwaka 2008, na kurejea Pakistan mwezi Marchi 2013.
Alikuwa na matumaini ya kukiongoza chama chake katika uchaguzi, lakini alikosa sifa ya kugombea na kujikuta akikabiliwa na mashitaka yanayomhusisha na uvunjaji wa sheria akiwa madarakani.
Musharraf mwenye umri wa miaka 70 amekuwa hospitali tangu mwanzoni mwa mwaka huu na taarifa zinasema anatibiwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Wafuasi wa Bwana Musharraf wamefanya maandamano katika mji wa Karachi wakitaka hukumu ya haki itendeke. Jaji amemsomea Bwana Musharraf mashitaka matano.
Amekana mashitaka yote lakini pia aliiambia mahakama mchango wake kwa nchi ya Pakistan na kuhoji vipi aitwe msaliti, akisema yeye ni mzalendo.
"Naitwa msaliti, Nimekuwa mkuu wa majeshi kwa miaka tisa na nimelitumikia jeshi hili kwa miaka 45. Nimepigana vita viwili na huu ni 'usaliti'?" Shirika la Habari la Ufaransa, AFP, limemkariri askisema.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA