Wednesday, March 12, 2014
0
Afrika Kusini imetoa onyo kali kwa Rwanda huku mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo ukiendelea kutokota.
Hii ni baada ya hali ya kulipiza kisasi kati ya nchi hizo katika kuwafurumusha mabalozi wao.
Alikuwa akigusia madai ya njama ya kumuua Generali Kayumba Nyamwasa, aliyekuwa anahudumu katika jeshi la Rwanda zamani ingawa sasa anaishi nchini Afrika Kusini.
Rwanda iliwafurusha wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini baada ya serikali ya Afrika Kusini kuwafukuza wafanyakazi watatu wa ubalozi wa Rwanda na mmoja wa Burundi nchini humo baada ya kuwahusisha na njama ya kutaka kumuua Nyamwasa.
Wakati huohuo, Mjumbe maalum wa Rais Barack Obama katika kanda ya maziwa makuu, Russ Feingold amesema kuwa nchi za Rwanda na Afrika Kusini hazina budi kumaliza mzozo kati yao kwa njia za kidiplomasia.
Mjumbe huyo aliyasema hayo mjini Kigali baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Feingold amesema Marekani inafuatilia kwa karibu karibu kundi la FDLR akilitaja kama moja ya makundi hatari katika eneo hilo la maziwa makuu.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA