Thursday, March 20, 2014
0
Waandishi wa habari nchini Rwanda

Serikali ya Rwanda imekanusha ripoti iliyochapishwa na shirika la kimataifa la waandishi wasio na mipaka kuihusu.
Ripoti hiyo imeishutumu Rwanda kwa kunyanyasa waandishi wa habari wa kimataifa pamoja na wale wa nchini humo ambao kwa miaka mingi hawajaweza...
kufanya kazi yao katika mazingira huru.
Aidha ripoti hiyo imeshutumu Rwanda kwa kutotoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu mazingira ya kikazi nchini humo.
 Afisa wa upashaji habari katika bodi ya kudhibiti habari na uandishi ya Rwanda Gerrard Mbanda amesema ripoti hiyo inalenga kuipaka matope serikali ya Rwanda.
Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano, ilisema kuwa serikali hutoa vitisho kwa waandishi wa habari na kutishia uhuru wa vyombo vya habari kufanya kazi zao.
Kadhalika shirika hilo limemtaka Rais Paul Kagame kuelewa, kuwa watu wanaweza kutumia njia sawa zinazokubalika kisheria kukosoa serikali bila ya kukiuka maadili na misingi ya serikali ya Rwanda.
Shirika hilo liliwataja waandishi kadhaa ambao lilisema wamenyanyaswa na serikali ya Rwanda.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA