Walioshuhudia shambulizi walisema kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha hilo.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa....
wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa na washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.
Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.
Inaarifiwa washambuliaji walitumia maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo.
poleni sana nduguzetu wa kenya, watanzania tupo pamoja ila naomba Rais Kenyatta ajipange na vyombo vya usalama waliangalie hilo kwani magaidi wamezidi sasa.
ReplyDeleteClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.