Waandishi hao ni pamoja na aliyekuwa mwandishi wa habari wa BBC, Peter Greste na Mohamed Fahmya ambaye alikuwa afisa mkuu wa Al Jazeera mjini Cairo.
Watatu hao waliruhusiwa kuongea na....
jaji ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu wazuiliwe.
Greste alimwambia jaji kuwa hawezi hata kutamka neno moja la kiarabu na madai dhidi yake kuwa alisaidia kundi la Brotherhood ni ya kushangaza sana.
Wamekuwa kizuizini tangu Disemba mwaka jana na mahakama kwa mara nyingine imewanyima dhamana.
Leo mahakama ilikuwa ichunguze ushahidi wa video, lakini hilo halikufanyika kwa sababu vifaa hivyo havikupatikana
Kesi yao imeahirishwa hadi tarehe 10 Aprili.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.